Posts

Image
  NA MWANDISHI WETU BENKI ya NMB, kupitia Program ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), imetoa msaada wa viti na meza 150 kwa shule za sekondari za Saranga ya Kimara na Mashujaa ya Sinza, pamoja na mabati 175 kwa shule ya msingi Mianzini, iliyopo Magomeni Makurumla, zote wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam, vyote vikiwa na thamani ya sh. 20 milioni. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jana Alhamisi ya Agosti 5, 2021 katika shule ya sekondari Saranga, ambako Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa NMB, Vicky Bishubo, alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Heri James, mbele ya Mbunge wa Ubungo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Kitila Mkumbo. Akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Bishubo amesema msaada huo ni sehemu ya utaratibu wao wa kila mwaka, ambako hutumia asilimia moja ya faida yao kwa mwaka uliotangulia, kurejesha kwa jamii kwa kusaidia utatuzi wa changamoto zinazoikabili Sekta za Elimu na Afya, pamoja na majanga.  Bishubo amebainisha kuwa, NMB inatambua, kuthamini na kuung

Wataalamu watoa tahadhari ya chanjo kwa wajawazito, wagonjwa

Image
  Awali, Balozi wa Marekani nchini, Dk. Donald Wright, akizungumza na Waandishi wa Habari Agosti 5, mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati wa maswali na majibu kwa waandishi wa habari. Na Faraja Masinde, Dar es Salaam WATANZANIA wanaendelea kuhimizwa juu ya kuchangamkia kupata chanjo ya kujikinga na virusi vya corona ambayo tayari imeendelea kutolewa kwenye maeneo mbalimbali nchini, hata hivyo kuna makundi ambayo watalaamu wa afya wameshauri yasipatiwe chanjo hiyo kwa sasa. Makundi hayo ni watoto chini ya miaka 18 na mtu anayeumwa. Wataalamu wa Afya wanaofanyakazi na Ubalozi wa Marekani nchini, kutoka kushoto ni Dk. Eva Matiko ambaye ni Bingwa wa Afya ya Jamii, akifuatiwa na Dk. Arkan Ibwe(katikati) na Dk. Emmanuel Tluway anayefanyakazi na Shirika la misaada la Marekani Usaid. Ushauri huo umetolewa na wataalamu wa afya wanaofanya kazi na Ubalozi wa Marekani nchini kwenye mkutano wa maswali na majibu kwa waandishi wa habari juu ya chanjo ya corona. Wameeleza sababu ya kutotolewa chanjo h

Bilioni 28 kulipa fidia watakaopisha bomba la mafuta kutoka Uganda

Image
  Mratibu wa Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania, Asiadi Murutu akizungumza na maafisa wa serikali mkoani Geita jana. PICHA Na Yohana Paul Geita. Na Yohana Paul, Geita TAKRIBANI Sh bilioni 28 zinatarajiwa kutumika kutoa malipo ya fidia kwa wananchi 10,516 nchi nzima watakaopisha utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi  (EACOP) kutoka nchini Uganda hadi mkoani Tanga. Maafisa wa Serikali Mkoani Geita wakipatiwa semina juu ya mradi wa bomba la mafuta Ghafi kutoka nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania. Hayo yameelezwa jana na Mratibu wa Mradi huo nchini, Asiadi Mrutu wakati wa semina kwa maafisa wa Serikali mkoani Geita iliyolenga kulenga kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa mradi, kujadili ushirikishwaji wa wananchi sambamba na kujadili fursa za mradi huo. Mrutu amesema fidia ya mradi huo ipo katika makundi mawili, kwanza ni maeneo ya yatakapojengwa makambi 14 na takribani wananchi 394 watalipwa fidia ya Sh bilioni 2.5 na ku

Wasanii waiangukia Serikali kuingilia kati soko la filamu

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo akizindua Filamu ya KOSA LA MAMA kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za kuendeleza tasnia ya uigizaji nchini. Na Yohana Paul, Geita WASANII wa Filamu mkoani Geita wameiomba Serikali kuendelea kuwaunga mkono na kuwawekea mazingira rafiki ya kuendeleza sanaa ikiwemo kuweka usimamizi madhubuti wa soko la filamu ambalo lina changamoto kubwa kwa sasa ili kuifanya tasnia ya uigizaji kutengeneza ajira kwa vijana. Akizungumza kwa niaba ya wenzake wakati wa uzinduzi filamu yake ya KOSA LA MAMA, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Maigizo ya Kapaya The Great, Michael Kapaya amesema serikali ikiweka usimamizi na kanuni thabiti kwenye soko la filamu. Amesema kw akufanya hivyo wataweza kujikwamu kiuchumi ambapo pia ameishauri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kuandaa matamasha ya filamu yatakayowasaidia wasanii kutangaza kazi zao. Aidha, Kapaya ameviomba vyombo vya habari kuipa nafasi sanaa ya uigizaji kama ilivyo kwa uimbaji kwani sanaa hiyo haiwez